MHE. Dkt. Nchemba Ateta Na Uongozi wa chuo cha ESAMI

September 2, 2024

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha ESAMI, Dkt. Peter Kiuluku.

Alieambatana na Meneja Mkazi wa Chuo hicho, Bw. Uli Mtebe, katika ofisi ya Waziri wa Fedha, jijini Dodoma, ambapo wamwejadiliana masuala mbalimbali ya ushikiriano kati ya Wiazara na Chuo hicho hususan mafunzo ya watumishi wa Wizara katika Chuo hicho ndani na nje ya nchi.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Christian Omolo, Mkurugenzi wa ldara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu, Bw. Lusius Mwenda na Mkurugenzi ldara ya Mipango, Bw. Moses Dulle.